Dr. Elimeleki Z. Katani profile
Biography
Nilizaliwa Mwanza, Katungulu mission. Nilisoma shule ya msingi Kazirikanda, Ukerewe.Nilisoma sekondari mwaka 1980, Kahololo Secondary school nikamaliza mwaka 1983. Mwaka 1986 nilijiunga na mafunzo ya Uganga, Masasi Mtwara na kumaliza mwaka 1988 nikaiunga JKT mwaka huo, Msange JKT na kujiunga 1989. Mwaka 1989 nilianza kufanya kazi Kolandoto hospitali kwa mhula wa mwaka mmoja. Mwaka 1990 nilijiunga na mafunzo ya Afisa tabibu, Sengerema hadi 1993 na nikaanza kufanya kazi tena katika hospitali ya Kolandoto mpaka 2001 nilipojiunga na masomo ya udaktari KCMC Moshi na kuhitimu 2005. Nikaanza kufanya kazi Makongoro kama mratibu wa afya ya msingi AICT. Mwaka 2004 nikajiunga na mafunzo ya udaktari wa magonjwa ya macho hadi 2006. Mwaka 2006, nikaajaliwa Kolandoto kama daktari bigwa wa magonjwa ya macho. Mwaka 2009 nikateuliwa kama mganga mkuu wa hospitali ya Kolandoto hadi mwaka 2016. Mwaka 2015, niliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa idara ya afya hadi sasa.