CHUO CHA UUGUZI MKULA CHAFUNGULIWA RASMI
Chuo cha Mafunzi ya uuguzi Mkula Hospital kwa jina la Bishop Kisula College of Health and Allied Sciences kiliwekewa jiwe la msingi na kufunguliwa rasmi tarehe 12/12/2013 na raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.
Tukio hili kubwa la kihistoria katika AICT lilifanyika kwenye eneo la chuo mbele ya ofisi ya administration.
Tukio hili liliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa kanisa akiwemo Askofu mkuu Silas Majaliwa Kezakubi, katibu mkuu Zakayo Bugota, Mkuu wa idara ya afya Dr Shadrack Watugala na viongozi mbalimbali wa kidini na serikali, pamoja na watu wote kwa ujumla.
Hospitali ya Mkula ni mmoja ya vituo vya afya vkubwa na tegemezi katika mkoa wa Simiu, imekuwa ikitoka mafunzo ya uuguzi ngazi ya cheti, kwa sasa Mkula itaweza kutoa mafunzo ya uuguzi kwa ngazi ya diploma.
Comments