Siku ya tatu: Eneo litakapo jengwa makao makuu ya AIC Burundi “LIVE”

Siku ya tarehe 3/5/2024 kikundi cha injili na misheni cha AICT kiliendelea na ziara yake ndani ya nchi ya Burundi. Mnamo saa Nne za asubuhi Viongozi wa AIC Burundi waliwapeleka wageni wao kwenye eneo la kiwanja sehemu inayoitwa Rubira, Bubanza kama kilometa 16 kutoka kituo cha kanisa la AIC Burundi zamani "ENGLISE EMMANUEL MIRACAL CENTER"  eneo walilopewa na serikali  wajenge makao makuu ya AIC Burundi. Kikundi kilifika na kuoneshwa eneo lenye ukubwa wa takribani wa urefu wa mita 200 na upana mita 100. Kiongozi wa AIC Burundi aliwaomba Viongozi wa AIC Tanzania wamsaidie kunjenga  Kanisa, Ofisi, Shule na Hospital.  Kabla ya kuondoka kwenye eneo la kiwanja kikundi cha Injili na Misheni kiliomba sara na baraka za Mungu akamilishe mipango na unjezi wa kanisa jipya la AIC Burundi.
Badaye viongozi wa kanisa la AIC Burundi waliwapeleka wageni mjini Bunjumbura ili wapate fursa ya kununua maitaji yao muhimu. Baadae mnamo saa 9 alasiri mwenyeji wao aliwakaribisha chakula cha mchana nyumbani kwake kabla ya kwenda kwenye ibada ya jioni.
Ibada:
Kiongozi wa Ibada hii alikuwa  Mch. Charles Bahebe Sanagu wa kanisa la AIC Changanyikeni - Dayosisi ya Pwani. Mhubiri alikuwa Mch. Musa Hezron wa AIC Magomeni - Dayosisi ya Pwani. Mhubiri alihubiri juu ya Nguvu ya Msalaba. Neno kuu lilitoka katika kitabu cha 1 Wakorintho 1:18 "Kwa sababu Neno la Msalaba kwao wanaopotea ni upiizi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu".  Mhubiri alisisitiza juu ya mambo manne kuhusu nguvu ya msalaba:
- Nguvu ya msalaba ina uwezo wa kubadilisha maisha ya watu
- Nguvu ya msalaba inatuwezesha kuishi maisha matakatifu
- Nguvu ya msalaba inatuwezesha kuendelea mbele katika imani bila kujali matatizo na misukosuko
- Nguvu ya msalaba hutuwezesha kumtumikia Mungu kwa mali zetu.


Mwishoni Mhubiri alitoa mwaliko kwa watu wenye mahitaji mbalimbali. Watu 31 walijitokeza ili waombewe. Baada ya maombi M/kiti wa ibada alifunga ibada.
Ibada ya Sinema
Ibada ya jioni iliongozwa na Mwinjilisti Stephen Kapongo. Filamu iliyooneshwa ni ya maisha ya Yesu.  Kabla ya onesho la sinema halijafika mwisho, kulitokea hitilafu ya umeme kiasi cha kuathiri mwisho wa filamu.

You must sign in to comment.Click Here to Sign In or Here to Register
Comments
    No comments found